Kenya miongoni mwa mataifa fisadi zaidi Afrika, duniani – ripoti
KENYA imeorodheshwa katika nafasi ya 137 duniani katika kupambana na ufisadi, huku ripoti mpya ikionyesha kudhoofika kwa uhuru wa mahakama na baadhi ya haki za kiraia.
Ripoti ya mwaka 2025 ya World Justice Project (WJP) Rule of Law Index inapatia Kenya nafasi ya 102 kati ya nchi na maeneo 143 duniani katika utekelezaji wa utawala wa sheria.
Alama ya jumla ya Kenya ilishuka kwa chini ya asilimia moja ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, lakini nchi ilifanya vibaya zaidi katika kipengele cha kupigana na ufisadi, ambapo iliorodheshwa ya 137 duniani na ya 31 kati ya nchi 34 za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kenya pia iliwekwa katika nafasi ya 128 duniani katika kipengele cha usalama na utulivu, hali inayoangazia changamoto za kulinda watu na mali yao.
Ripoti hiyo inasema mifumo ya kuzuia matumizi mabaya ya mamlaka na kuhakikisha taasisi za serikali zinawajibika imeendelea kudhoofika.
“Uadilifu wa mifumo ya kuzuia na kusawazisha mamlaka pia umedhoofika pakubwa, ikiwemo nchini Kenya,” ripoti hiyo inasema.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa uhuru wa kutoa maoni, kujieleza, kukusanyika na kujiunga na mashirika umepungua katika baadhi ya nchi, Kenya ikiwa miongoni mwa zilizorekodi kushuka katika vipengele hivyo.
Hata hivyo, ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiraia nchini Kenya ulisalia bila mabadiliko makubwa, tofauti na mataifa mengi ambako ushiriki huo ulipungua.
Ripoti hiyo pia inaonyesha wasiwasi kuhusu kuingiliwa kwa mifumo ya haki na wanasiasa. Kenya ilishuka katika vipimo vinavyochunguza uwezo wa mahakama kuzuia matumizi mabaya ya mamlaka ya serikali kuu na uhuru wa mifumo ya haki ya kesi za jinai.
Licha ya changamoto hizo, Kenya ilifanya vizuri zaidi katika baadhi ya vipengele. Ilishika nafasi ya 69 duniani katika uwazi wa serikali, ya 82 katika haki za madai na ya 87 katika haki za jinai.
Uwazi wa serikali ulijumuisha upatikanaji wa taarifa za umma na mifumo inayowawezesha wananchi kuwawajibisha viongozi. Hiki ndicho kilikuwa kipengele kilichopatia Kenya matokeo bora zaidi kati ya vipengele vinane vilivyopimwa.
WJP hutumia maoni ya wananchi, wanasheria na wataalamu kutathmini jinsi utawala wa sheria unavyotekelezwa katika maisha ya kila siku, badala ya kutegemea Katiba na sheria pekee.
Duniani kote, asilimia 68 ya nchi na maeneo 143 yaliyotathminiwa yalirekodi kushuka kwa viwango vya utawala wa sheria mwaka 2025, ikilinganishwa na asilimia 57 mwaka 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa WJP Alejandro Ponce alisema hali hiyo imegeuka kwa kasi baada ya kushuka kwa viwango hivyo katika miaka iliyotangulia.
“Kuharibiwa kwa taratibu za utawala wa sheria kulipungua katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, mwaka huu tunaona mabadiliko makubwa, huku nchi nyingi zaidi zikishuka na chache zikiimarika,” alisema.
Denmark iliongoza katika orodha ya kimataifa, ikifuatiwa na Norway, Finland, Sweden na New Zealand, huku Venezuela ikiwa ya mwisho.
Katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya ilishika nafasi ya 13 kati ya nchi 34, na nafasi ya 15 kati ya nchi 35 zenye uchumi wa kipato cha chini-kati.
Matokeo hayo yanaangazia changamoto ya kuhakikisha kuwa haki zilizowekwa katika Katiba zinalindwa, taasisi za umma zinawajibika na mamlaka yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.