Kenya kutamba katika biashara ya mafuta Afrika Mashariki na Kati kupitia kiwanda kipya cha Dangote
MRADI wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta cha Dangote kinachotarajiwa kujengwa Lamu unatazamiwa kubadilisha nafasi ya Kenya katika biashara ya mafuta huku ukipatia Afrika Mashariki uwezo mkubwa wa kujitosheleza kwa bidhaa za petroli.
Kiwanda hicho cha thamani ya zaidi ya Sh2 trilioni kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku, kiwango kinacholingana na uwezo wa Kiwanda cha Dangote nchini Nigeria ambacho sasa ni miongoni mwa vikubwa zaidi duniani.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Petroli nchini, Joseph Otieno, mapipa 700,000 kwa siku yanamaanisha kiwanda hicho kitakuwa kinatumia mafuta ghafi ya zaidi ya lita 111 milioni kila siku ili kuzalisha petroli, dizeli, mafuta ya ndege, gesi ya LPG, mafuta mazito na lami.
Wataalamu wanasema uwezo huo ni mkubwa ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya mafuta katika Afrika Mashariki ambayo yanakadiriwa kuwa mapipa 450,000 kwa siku. Hii ina maana kuwa kiwanda hicho kitaweza kukidhi mahitaji yote ya Kenya na bado kisambaze mafuta katika nchi jirani.
Kwa sasa Kenya pamoja na masoko ya kanda yanayohudumiwa na kampuni zake za mafuta hutumia takriban lita 21 milioni za petroli, dizeli na mafuta ya ndege kwa siku. Hata hivyo, kiwanda cha Lamu kinatarajiwa kuzalisha zaidi ya lita100 milioni za bidhaa hizo kila siku.
Serikali inaamini uwekezaji huo utaimarisha usalama wa upatikanaji wa mafuta na kupunguza kutegemea bidhaa za petroli kutoka nje ya bara la Afrika. Pia utasaidia nchi za eneo hili kukabiliana na misukosuko ya soko la kimataifa na changamoto za usafirishaji wa mafuta.
Mbali na mafuta ya kawaida, kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha kemikali za viwandani zinazotumiwa kutengeneza plastiki, mbolea, vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine nyingi za viwandani.
Mradi huo pia unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya Kaunti ya Lamu. Ujenzi wake utahitaji nyumba, hospitali, vituo vya mafunzo, mabohari, maabara, huduma za mawasiliano na miundombinu mingine muhimu.
Katika kipindi cha miaka mitatu ya ujenzi, mafundi wataweka mashine za kusafisha mafuta, matangi makubwa ya kuhifadhi bidhaa, mabomba ya usafirishaji, mifumo ya umeme, maji na usalama pamoja na vituo vya kupokea mafuta kutoka meli na kusafirisha bidhaa zilizokamilika.
Wataalamu wanaeleza kuwa uwekezaji wa Sh2 trilioni ni sawa na karibu asilimia 12 ya Pato la Taifa la Kenya, jambo linaloonyesha ukubwa wa mradi huo. Ikiwa utekelezaji wake utafanikiwa, Lamu inaweza kuwa mojawapo ya vituo vikuu vya biashara ya mafuta na viwanda katika Afrika Mashariki na Kati.