Kajuna, Kahama Madini zafuzu First League
Timu za Kajuna ya Kigoma na Kahama Madini ya Shinyanga, zimekata tiketi ya kushiriki Ligi Daraja la Pili (First League) msimu ujao baada ya leo Alhamisi, Aprili 30, 2026, kuibuka na ushindi katika mechi zao za nusu fainali za mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zilizochezwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.