Julius Kyazze atambuliwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi Afrika
MWANABIASHARA wa sekta ya ubunifu na burudani kutoka Uganda, Julius Kyazze, ametambuliwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.
Kyazze, ambaye ni mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa LIVE54+, alitunukiwa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika Kigali, Rwanda, Septemba 25, 2026.
Alikuwa mwakilishi pekee wa sekta ya ubunifu miongoni mwa viongozi waliotambuliwa katika nyanja mbalimbali.
Kutambuliwa kwake kunafuatia zaidi ya miongo miwili ya shughuli za ujasiriamali katika sekta za ubunifu, burudani, vyombo vya habari na michezo barani Afrika.
Kyazze amehusika katika kujenga na kuendesha biashara Uganda, Kenya, Tanzania, Ghana na Rwanda, huku akishirikisha wataalamu na wadau kutoka masoko mbalimbali.
Kupitia LIVE54+, amekuwa akihusishwa na shughuli zinazohusu vyombo vya habari, ubunifu, uzoefu wa chapa, maudhui, vipaji na uzalishaji wa kazi za burudani.
Katika taarifa yake, LIVE54+ ilisema kutambuliwa kwa Kyazze kunaangazia mchango wa wafanyabiashara katika kukuza sekta ya ubunifu barani Afrika.
“Kyazze amejikita katika kujenga biashara,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kutambuliwa kwake pamoja na viongozi kutoka sekta nyingine kunaweka biashara za ubunifu katika mjadala mpana kuhusu ushawishi na maendeleo ya bara.
LIVE54+ ni kundi la biashara za Kiafrika zinazofanya kazi katika sekta za vyombo vya habari, ubunifu, maudhui, vipaji na uzalishaji.