Jinsi ya kupika mlo mtamu wa mchuzi wa samaki kwa viungo

Taifa Leo
Published: Oct 11, 2026 15:40:25 EAT   |  General

MAPISHI KIKWETU

Jinsi ya kupika mlo mtamu wa mchuzi wa samaki kwa viungo

MAHITAJI

Samaki 2

Mafuta ya kupikia

Chumvi

Limau au ndimu kubwa 1

Kitunguu maji kikubwa 1

Nyanya 4

Tomato paste vijiko vikubwa 2

Fish Masala

Hoho jekundu kubwa 1

Hoho ya kijani kibichi kubwa 1

Tangawizi iliyosagwa kijiko kikubwa 1

Kitunguu thomu

Pilipili ya unga (hiari) kijiko kidogo ½

Pilipili manga vijiko vikubwa 2

Binzari nyembamba kijiko kidogo 1

Binzari ya manjano kijiko kidogo 1

Mbegu za haladari kijiko kidogo 1

Maandalizi

Safisha samaki na ukatekate minofu.

Katika karai kubwa safi, weka minofu ya samaki, miminia chumvi kiasi, masala, tangawizi, kitunguu thomu, pilipili manga.

Kamua limao au ndimu kisha uchanganye vyema samaki na viungo.

Weka kando na usubiri kwa saa moja ili viungo vikolee.

Asha moto, bandika kikaangio safi kisha umimine mafuta kiasi.

Subiri yapate moto kwenye moto wa wastan kisha kaanga minofu ya samaki hadi igeuke rangi nzuri ya kahawia.

Chukua sufuria nyingine safi na ubandike kwenye moto wa wastan, weka mafuta na usubiri yawe moto.

Mimina mbegu za haladari na ukoroge, ongeza kitunguu maji, koroga hadi vilainike

Tia binzari nyembamba, kitunguu thomu, tangawizi iliyopondwa na ukoroge viungo vichanganyike vyema hadi vitoe harufu tamu.

Weka binzari ya manjano, pilipili nyekundu, hoho zilizokatwakatwa, koroga hadi vilainike.

Mimina rojo la nyanya na ukoroge viungo vyote, funika na usubiri kwa dakika tano nyanya ziive.

Ongeza samaki ulizochoma, changanya viungo na tomato paste.

Kamulia limao moja, weka chumvi kiasi na uongeze maji kiasi cha haja.

Funika kwa dakika tano zitokote kwa moto wa chini.

Kitoweo cha mchuzi wa samaki wenye viungo kipo tayari.

Unaweza kuambatisha kwa wali au sima na sharubati baridi.