Harambee Stars kupepetana na wanyonge Chad mechi ya kirafiki

KOCHA wa Harambee Stars Benni McCarthy Jumamosi atakuwa akilenga kupata ushindi wake wa kwanza timu hiyo ikipepetana na wanyonge Chad kwenye mechi ya kirafiki uwanja wa Marrakech, Morocco.
Mchuano huo ambao unatarajiwa kuanza saa 12 jioni, utakuwa wa kwanza kati ya Kenya na Chad. Pia timu hizo mbili zitapepetana katika mechi nyingine ya kirafiki mnamo Jumanne wiki ijayo.
Tangu kuteuliwa kwake kama kocha wa Harambee Stars mnamo Machi 3, McCarthy, 48 ameongeza Kenya katika mechi mbili. Michuano hiyo ilikuwa sare ya 3-3 dhidi ya wenyeji Gambia na kupigwa 2-1 nyumbani na Gabon katika mtanange wao wa Kundi F, 2026, mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Katika viwango vya orodha ya Fifa, Kenya wapo nafasi 111 huku Chad ikiwa nambari 177. Mechi hizo mbili zitakuwa sehemu ya maandalizi ya Kenya kwa kipute cha Ubingwa wa Afrika kwa wanasoka wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN 2024).
Kenya, Uganda na Tanzania wataandaa kipute hicho ambacho kimeratibishwa kitaanza mnamo Agosti 2 hadi 30 na kwa sasa mataifa yote matatu yanaendelea na maandalizi yake.
Ni wachezaji wanne tu kwenye kikosi cha McCarthy cha wanasoka 23 ambao wanasakata soka kwenye ligi za nje. Wanne hao mnyakaji Brian Bwire (Polokwane City FC, Afrika Kusini), beki mzoefu Brian Mandela (Stellenbosch FC, Kusini) na kiungo Adam Wilson (The New Saints FC, Uingereza) kisha William Lenkupae (Central Coastal Mariners FC, Australia).
Beki wa Bandari Swaleh Pamba ndiye mchezaji mgeni pekee kwenye timu hiyo. Mechi hizo za kirafiki pia zitakuwa za kwanza kwa Anthony Kimani kufuatia uteuzi wake kama naibu kocha wa Harambee Stars mnamo Aprili.
Kwa kuwa mshambulizi Michael Olungo hayuko kwenye kikosi, safu ya mbele huenda itaongozwa na Beja Nyamawi, (Bandari), Moses Shumah (Kakamega Homeboyz) na Emmanuel Osoro (FC Talanta).