Fei Toto: Watanzania wamefurahi

Mwanaspoti
Published: Aug 02, 2025 19:24:01 EAT   |  Sports

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Feisal Salum 'Fei Toto' amesema ni fahari kwa kikosi hicho kuanza vyema fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN), baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso.