Fedha za kilimo zinufaishe wakulima wa mashamba madogo

Taifa Leo
Published: Jul 19, 2026 17:40:33 EAT   |  General

MASHIRIKA ya kifedha yamehimizwa kubuni upya huduma za ufadhili wa kilimo ili ziambatane na hali halisi ya wakulima, vijana, wanawake wajasiriamali na masoko ya chakula badala ya kuzingatia utoaji wa mikopo pekee.

Wito huo ulitolewa wakati wa mkutano wa Financing Agri-Food Systems Sustainably (FINAS) 2026 uliofanyika Nairobi chini ya kaulimbiu “Towards Sustainable Financial Architecture for Africa’s Food Systems.”

Mkutano huo ulileta pamoja serikali, taasisi za kifedha, washirika wa maendeleo na wadau wa kilimo kujadili mbinu za kuwekeza katika mifumo imara ya chakula.

Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Kenya, Wairimu Munyinyi-Wahome, alisema huduma za kifedha zinapaswa kuzingatia misimu ya uzalishaji, uwezo wa biashara, fursa za masoko na hatari zinazowakabili wakulima.

[caption id="attachment_190271" align="aligncenter" width="300"] Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Kenya, Wairimu Munyinyi-Wahome akizungumza jijini Nairobi. Picha|Sammy Waweru[/caption]

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukihoji kama wakulima wanafaa kupewa mikopo. Swali muhimu ni kama mifumo yetu ya kifedha iliundwa kuambatana na uhalisia wa kilimo,” alisema.

Aliongeza kuwa mfumo bora wa kifedha unapaswa kuendana na kilimo, badala ya kulazimisha wakulima kufuata masharti magumu kama dhamana, ratiba zisizobadilika za malipo ya mikopo na historia rasmi ya mikopo.

Kwenye kongamano na FINAS 2026, Heifer ilieleza kuwa imejikita katika kuunganisha ufadhili na ujuzi, kuongeza uzalishaji, kuimarisha usawa wa kijinsia katika huduma za kifedha na kusaidia vijana pamoja na wakulima wadogo kupata uwekezaji wa kibiashara.

Mkurugenzi Mkuu wa Heifer Rwanda, Verena Ruzibuka, alisema ubunifu mwingi unaoanzishwa na vijana unahitaji msaada zaidi ili kukua na kuwa biashara zinazowanufaisha wakulima. “Mpango wa AYuTe Africa NextGen unaowapa wabunifu wa teknolojia za kilimo ufadhili, mafunzo, ushauri na masoko, umeonyesha jinsi ya kufadhili wakulima,” alitaja.

[caption id="attachment_190274" align="aligncenter" width="300"] Baadhi ya wakulima walionufaika mwaka huu 2026 kupitia mpango wa AYuTE wa Heifer Kenya ambao hulenga kupiga jeki vijana wenye bunifu mbalimbali za kilimo. Picha|Sammy Waweru[/caption]

Mkurugenzi wa Ubunifu wa Fedha wa Heifer Afrika, Wangui Muna, alisema matumizi ya teknolojia na takwimu sahihi yatapunguza hatari za utoaji wa mikopo na kuongeza upatikanaji wa bidhaa za kifedha zinazofaa sekta ya kilimo.

Mkutano huo pia ulitumika kuzindua Agricultural Finance Technical Working Group, kundi la kiufundi la fedha litakalosaidia kuimarisha sera na kanuni za ufadhili wa kilimo kwa kutumia ushahidi wa kisayansi.

Aidha, kundi hilo linaongozwa na Kenya Bankers Association kwa ushirikiano na GIZ, FSD Kenya, Africa Guarantee Fund, Heifer International na Aceli Africa.

Mkurugenzi wa Sera wa Aceli Africa, Titianne Donde, alisema taarifa na takwimu zilizopo zinapaswa kutafsiriwa kuwa sera zitakazochochea uwekezaji katika kilimo.

[caption id="attachment_190275" align="aligncenter" width="300"] Heifer Interntanional inahimiza mashirika ya kifedha kubuni upya huduma za ufadhili wa kilimo ili ziambatane na hali halisi ya wakulima, vijana, wanawake wajasiriamali na masoko ya chakula badala ya kuzingatia utoaji wa mikopo pekee. Wengi wa wanaokuza kabichi ni wakulima wa mashamba madogo hivyo basi wanahitaji kupigwa jeki kifedha. Picha|Sammy Waweru[/caption]

Kulingana na Wairimu Munyinyi-Wahome, Heifer itaendelea kushirikiana na wadau kubuni mifumo ya kifedha itakayowawezesha wakulima, vyama vya ushirika, wanawake na vijana kujenga biashara imara na endelevu.