Faida za nishati ya jua katika kilimo

Taifa Leo
Published: Aug 17, 2026 09:48:09 EAT   |  Sports

KWA wakulima wanaotumia mfumo wa umwagiliaji maji mashamba na mimea kwa kutumia mifereji, gharama ya nishati inaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kuongeza uzalishaji na faida. Hata hivyo, matumizi ya nishati ya jua yanaibuka kama suluhisho kupunguza gharama huku yakihakikisha upatikanaji wa maji shambani. Esther Wariara Ng’ang’a, mkulima kutoka Kiairia, Githunguri, Kaunti ya Kiambu, ni mmoja wa wakulima wanaonufaika na teknolojia hiyo. Kabla ya kutumia pampu ya sola, alitumia takriban Sh500 kila siku kulipia umeme wa kupampu maji kutoka kisimani. “Sasa natumia karibu Sh250 pekee kwa siku. Fedha ninazookoa nazirejesha shambani kwa kuongeza uzalishaji,” anasema. [caption id="attachment_191214" align="aligncenter" width="300"] Esther Wariara Ng’ang’a, mkulima kutoka Kiairia, Githunguri, Kaunti ya Kiambu anayetumia nishati ya jua kuendeleza kilimo. Picha|Sammy Waweru[/caption] Mbali na kupunguza gharama, nishati ya jua imemwezesha Esther kupata maji ya umwagiliaji mimea bila kukosekana. Hali hii imemsaidia kumwagilia mimea maji wakati yanapoyahitaji, badala ya kutegemea mvua. “Matokeo yake ni ongezeko la mavuno. Kabla ya kutumia pampu ya sola, nilikuwa nikivuna karibu kilo 50 za managu kwa wiki. Sasa huvuna takriban kilo 200 kwa wiki,” anaambia ‘Akilimali Dijitali’. Pia huvuna karibu kilo 50 za terere na kilo 100 za sukuma wiki kila wiki, kulingana na mahitaji ya soko. Esther huuza managu na terere kwa Sh50 kwa kilo, huku akiuza zaidi ya kilo 500 za ndizi kwa mwezi kwa Sh45 kwa kilo. “Hulima ndizi na tuna chama cha ushirika kinachotusaidia kupata soko lenye ushindani mkuu,” akasema wakati wa mahojiano shambani mwake Githunguri. [caption id="attachment_191215" align="aligncenter" width="300"] Tangi la maji ambalo Esther Wariara Ng'ang'a hupampu maji kwa kutumia sola. Picha|Sammy Waweru[/caption] Pampu ya sola aliipata baada ya kupata mafunzo kuhusu teknolojia za nishati safi kupitia mradi wa Anglican Development Services (ADS) Mount Kenya. Alilipa Sh19,000, ada za kwanza, na sasa hulipa Sh4,000 kila mwezi kwa mwaka mmoja, huku gharama ya mfumo mzima ikiwa Sh67,000. Anasema nishati ya jua imempunguzia gharama za uzalishaji, kuongeza mavuno na kumpa nafasi ya kuwekeza zaidi katika shamba. Lengo lake sasa ni kutumia nishati safi katika shughuli zote za shamba, ikiwemo biogas ya mapishi, ili kupunguza gharama zaidi.  