Enez Mango sasa ni mali ya Politehnica Timișoara Feminina ya Romania

Taifa Leo
Published: Sep 27, 2026 17:44:55 EAT   |  Sports

BEKI wa Harambee Starlets, Enez Mango, amejiunga na klabu ya Politehnica Timișoara Feminina ya Romania baada ya kuitumikia Farul Constanța ya Romania kwa miaka minne.

Mango, ambaye ni beki wa kushoto, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Divisheni ya Pili ya Wanawake nchini Romania, ukiwa na kipengele cha kuongeza muda wake.

Akizungumza kipekee na Taifa Spoti, Mango hakuficha furaha yake kujiunga na klabu hiyo, akisema atapata fursa ya kucheza tena pamoja na kiungo Laura Rus, ambaye anamtaja kuwa mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea katika soka ya Romania.

“Nina furaha kubwa kwa sababu Laura Rus, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora katika historia ya soka la Romania, yupo hapo. Nilicheza naye Farul, lakini aliondoka mapema. Kucheza naye tena ni jambo la kufurahisha kwa sababu tulikuwa na maelewano mazuri sana uwanjani,” alisema Mango.

Aliongeza: “Politehnica ni klabu kubwa, na pia ninapenda jiji hilo pamoja na mazingira na hali za timu.”

Mango anatarajiwa kujiunga na wenzake pindi atakapopata visa ya kwenda Romania.

Beki huyo mwenye uzoefu pia alikuwa akivutia vilabu vingine viwili vya Romania, Gloria na Timișoara, kabla ya kuamua kujiunga na Politehnica.

Klabu hiyo yenye makao yake katika jiji la Timișoara, magharibi mwa Romania, ilianzishwa mwaka 1921 na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Timișoara. Kwa sasa inapigania kupanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini humo msimu ujao.

Uhamisho huo unamfungulia Mango ukurasa mpya katika soka ya kulipwa barani Ulaya, baada ya kipindi chenye mafanikio akiwa na Farul Constanța, ambako pia ni nyumbani kwa mlinda lango wa Starlets, Lilian Awuor.

Mango alijiunga na Farul mwaka 2022 akitokea Vihiga Queens, ambapo alikuwa nahodha na mmoja wa wachezaji tegemeo wa timu hiyo.

Akiwa Farul, alishinda mataji mawili ya ligi na kuhudumu kama nahodha. Pia alishiriki katika mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa Wanawake (UEFA ), ambako alicheza pamoja na Awuor.

Kabla ya kuhamia Romania, Mango alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Vihiga Queens, akiiongoza kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF-WPL).

Pia aliiongoza Vihiga Queens kutwaa ubingwa wa mashindano ya Klabu Bingwa ya Wanawake ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) mwaka 2021. Ushindi huo uliiwezesha timu hiyo kufuzu kwa mara ya kwanza kwa Klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake.

Mango, 33, amekuwa mchezaji wa Starlets tangu mwaka 2015, akishiriki katika mechi mbalimbali za kimataifa, zikiwemo kuwakilisha Kenya katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON).

Alikuwa sehemu ya kikosi cha Kenya kilichoshiriki fainali za WAFCON nchini Morocco mwaka huu, ambapo Starlets ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji Morocco, Algeria na Senegal lakini Kenya ikabanduliwa mapema baada ya kupoteza mechi zote za hatua ya makundi.

Uzoefu wake wa soka ya ndani na kimataifa unatarajiwa kuwa muhimu anapoanza safari mpya na Politehnica Timișoara, huku akilenga kusaidia klabu hiyo kupanda daraja na kufikia malengo yake ya kushiriki michuano ya UEFA.