DPP akataa mpelelezi wa Uingereza kutoa ushahidi katika kesi ya ulanguzi mihadarati

Taifa Leo
Published: Sep 18, 2026 06:55:18 EAT   |  News

KIONGOZI wa Mashtaka ya Umma ameaomba mpelelezi wa zamani wa kitengo cha polisi cha Uingereza (Scotland Yard) azuiliwe kutoa ushahidi katika kesi ya ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya methamphetamine yenye thamani ya Sh8.2 bilioni iliyowakabili raia sita wa Iran.

Upande wa mashtaka ulisema mpelelezi huyo wa zamani, Bw Kevin Hurley, hakuhusika katika kukamatwa kwa dawa hizo wala uchunguzi wa kesi hiyo, hivyo hakuwa na msingi wa kutoa ushahidi kuhusu masuala yaliyohusiana na kesi hiyo.

Bw Hurley alikuwa miongoni mwa mashahidi ambao washtakiwa hao walikuwa wamepanga kuwaita ili kupinga ushahidi wa upande wa mashtaka.

Ushahidi wake ulitarajiwa kuangazia namna dawa hizo za kulevya zilizodaiwa kukamatwa katika Bahari Hindi zilivyopaswa kukusanywa, kuhifadhiwa, kutambuliwa, kuhamishwa, kupimwa, kuchunguzwa katika maabara na hatimaye kuwasilishwa mahakamani.

Ushahidi wake pia ulilenga kuchunguza iwapo dawa hizo zilishughulikiwa ipasavyo tangu zilipokamatwa baharini, zilipokabidhiwa kwa mamlaka za Kenya, zilipohifadhiwa, kupimwa uzito, kuchukuliwa sampuli na hatimaye kuwasilishwa mahakamani.

Upande wa mashtaka ulipinga vikali ushahidi wake, ukisema Bw Hurley hakuwa akiwasilishwa kama shahidi mtaalamu na akauliza msingi wake kutoa ushahidi kuhusu masuala yaliyohusiana na kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa, kupitia kwa wakili wao, walipinga hoja hiyo wakisema upande wa mashtaka haukutoa sababu za msingi kisheria kumzuia Bw Hurley kutoa ushahidi kabla ya mahakama kumsikiliza.

Wakili wa washtakiwa alisema Bw Hurley hatatoa ufasiri wa sheria za Kenya wala kusimulia kilichotokea wakati wa kukamatwa kwa dawa hizo.

“Atatoa maoni yake ya kitaalamu kuhusu iwapo taratibu zilizotumika kushughulikia dawa hizo zinazodaiwa kuwa za kulevya zilifuata viwango vinavyotambulika vya utunzaji, uhifadhi na uwasilishaji wa ushahidi,” akaeleza.

Mahakama itaamua wiki ijayo kama Bw Hurley atakubaliwa kutoa ushahidi wake au la.

Jaseem Darzadeh Nia, Nadeem Jadgal, Hassan Baloch, Raheem Baksh, Imran Baloch na Imtiyaz Daryay wanakabiliwa na shtaka la kuhusika katika ulanguzi wa kilo 1,036.044 za methamphetamine zenye thamani ya takriban Sh8.2 bilioni.

Wiki iliyopita, Mahakama ya Shanzu iliamua kuwa watu hao wana kesi ya kujibu baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi unaowataka washtakiwa hao kujitetea.

Mahakama ilisema ushahidi huo ulihusisha operesheni iliyofanyika katika bahari kuu na ulihusisha meli iliyodaiwa kubeba zaidi ya tani moja ya methamphetamine.

Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa mashahidi 12, wakiwemo wanajeshi wa Jeshi la Wanamaji waliohusika katika kukamatwa kwa dawa hizo, wataalamu kutoka Maabara ya Serikali na nyaraka mbalimbali za ushahidi.

Washtakiwa hao walikiri kosa walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, lakini baadaye walikanusha shtaka hilo.

Walidai kupitia mkalimani kuwa dawa hizo zilikuwa na uzito wa takriban kilo 800, wakisema wachunguzi walihesabu pia uzito wa vifungashio.

Pia walidai kuwa methamphetamine ilikuwa halali nchini mwao na haikukusudiwa kutumiwa vibaya.

Washtakiwa hao wamekuwa kizuizini tangu walipokamatwa mwaka jana baada ya kunyimwa dhamana.