Dodoma kuzindua kitabu cha kukuza utalii

DODOMA: OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Ulinzi na Usalama ya Sekta ya Utalii Tanzania (TTSSP) inakusudia kuzindua kitabu cha mkakati za kukuza utalii wa mkoa huo, tukio litakalofanyika Agosti 4, 2025 saa 3:00 asubuhi ukumbi wa Mabeyo Complex Dodoma. Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo na kusainiwa na Mkuu …
DODOMA: OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Ulinzi na Usalama ya Sekta ya Utalii Tanzania (TTSSP) inakusudia kuzindua kitabu cha mkakati za kukuza utalii wa mkoa huo, tukio litakalofanyika Agosti 4, 2025 saa 3:00 asubuhi ukumbi wa Mabeyo Complex Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo na kusainiwa na Mkuu wa Mkoa, Rosemary Senyamule imeeleza mgeni rasmi kwenye tukio hilo atakuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi. Mahmoud Thabiti Kombo.
“Ninayofuraha kubwa kuwaalika nyote kwa ajili ya uzinduzi muhimu wa kitabu cha “Mkakati wa Kuendeleza Utalii mkoani Dodoma”. Mkakati huu unaashiria sura mpya muhimu katika kukuza sekta ya utalii ndani ya Mkoa wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla,” imeeleza taarifa hiyo.
SOMA ZAIDI
Zaidi ya mil 400 kusambaza mitungi ya gesi Dodoma