CRDB Marathon yavuka Sh5 bilioni

Mwanaspoti
Published: Aug 16, 2026 13:35:13 EAT   |  Sports

MASHINDANO ya CRDB Bank International Marathon, yamegeuka kutoka kuwa tukio la michezo na kuwa mpango mkubwa wa kuleta athari chanya katika jamii, baada ya kukusanya zaidi ya Sh5 bilioni tangu yalipoanzishwa mwaka 2020, fedha ambazo zimeelekezwa katika kuboresha huduma za afya, kuwawezesha vijana na maendeleo ya jamii nchini Tanzania.