CCM yaja na mpango kuboresha barabara Moro

MOROGORO: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuwa endapo kikipata ridhaa ya kuongoza tena miaka mitano ijayo, kitaanza kusuka upya miundombinu ya barabara mkoani Morogoro. Ujenzi huo utakuwa wa kiwango cha lami barabara 25, kati ya hizo 17 zikiwa za kiwango cha changarawe na nane za lami zenye jumla ya kilometa 827.6. Mgombea Mwenza wa Urais …
The post CCM yaja na mpango kuboresha barabara Moro first appeared on HabariLeo.
MOROGORO: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuwa endapo kikipata ridhaa ya kuongoza tena miaka mitano ijayo, kitaanza kusuka upya miundombinu ya barabara mkoani Morogoro.
Ujenzi huo utakuwa wa kiwango cha lami barabara 25, kati ya hizo 17 zikiwa za kiwango cha changarawe na nane za lami zenye jumla ya kilometa 827.6.
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema hayo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Mikumbi mkoani Morogoro.
Alisema uboreshaji na ujenzi huo wa barabara ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2025/2030.
Alisema serikali itatekeleza mpango huo ili kufungua zaidi fursa za biashara, kilimo, ufugaji na utali.
The post CCM yaja na mpango kuboresha barabara Moro first appeared on HabariLeo.