CCM Tanga shwari, Sh Bil 35 kupeleka maji Mkinga
TANGA; Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimeridhishwa na uhai na utekelezaji wa shughuli za chama Mkoa wa Tanga kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya chama na serikali umesaidia kurahisisha upelekaji wa maendeleo kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi katika ziara yake mkoani Tanga …
TANGA; Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimeridhishwa na uhai na utekelezaji wa shughuli za chama Mkoa wa Tanga kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya chama na serikali umesaidia kurahisisha upelekaji wa maendeleo kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi katika ziara yake mkoani Tanga yenye lengo la kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025-2030.
Kihongosi amesema changamoto kubwa inayowakabili wananchi wa Mkinga ni suala la upatikanaji wa maji, lakini Rais Dk Samia Suluhu Hassan ametoa Sh bilioni 35 kwa ajili ya mradi wa maji.
“Changamoto kubwa inayowakabili hapa ni changamoto ya maji lakini hapa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameletea bilioni 35 za mradi wa maji,” amesema Kihongosi.
Akizungumza wakati akizindua Shina Namba 6 lililopo Mbuyuni, Kata ya Manza, Kihongosi amesema wananchi wamekuwa wakipata changamoto za maji, afya, elimu na nyinginezo lakini serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais Samia imekuwa macho kuhakikisha inawaletea wananchi maendeleo.
–