CCM kuifanya hospitali ya Mkapa kuwa ya kimataifa

MOROGORO: Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema Serikali ya CCM imepanga kuibadilisha Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kuwa kituo bora cha kimataifa cha mafunzo, huduma za kibingwa na utafiti wa kitabibu katika miaka mitano ijayo endapo itapata ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi. Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Nkuhungu jijini Dodoma, …
The post CCM kuifanya hospitali ya Mkapa kuwa ya kimataifa first appeared on HabariLeo.
MOROGORO: Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema Serikali ya CCM imepanga kuibadilisha Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kuwa kituo bora cha kimataifa cha mafunzo, huduma za kibingwa na utafiti wa kitabibu katika miaka mitano ijayo endapo itapata ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi.
Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Nkuhungu jijini Dodoma, Dk. Nchimbi alisema hospitali hiyo itawezesha kufundisha madaktari, wauguzi na wataalamu wa afya kutoka ndani na nje ya nchi, sambamba na kuongeza huduma za kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Aidha, akizungumzia sekta ya nishati, Dk. Nchimbi alisema uongozi wa Rais Samia umefanya mageuzi makubwa, ikiwemo kukamilisha ufungaji wa mitambo katika Bwawa la Mwalimu Nyerere na kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 1,602 hadi 3,078, pamoja na kufikisha umeme katika vijiji vyote 12,318 vya Tanzania.
Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kumpa kura Rais Dk. Samia pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani wa CCM ili kazi ya maendeleo iendelee.
The post CCM kuifanya hospitali ya Mkapa kuwa ya kimataifa first appeared on HabariLeo.