Bunge lapitisha sheria kutatua msongamano shule za kitaifa
SHULE za jamii, zilizo katika kundi la C4, huenda zikanufaika pakubwa na mpango mpya wa usajili wa wanafunzi wa Gredi 10 unaopendekezwa kuanza Januari 2027.
Wabunge wamepitisha kwa kauli moja hoja inayotaka Wizara ya Elimu, kwa ushirikiano na taasisi nyingine, kuweka idadi ya mikondo ambayo kila kundi la shule linaweza kuwa nayo.
Chini ya pendekezo hilo, shule za kitaifa zilizo kundi la C1 zitakuwa na mikondo isiyozidi 10, za mikoa zilizo kundi la C2 mikondo minane, za kiwango cha kaunti katika kundi la C3 mikondo mitano na za kaunti ndogo na kijamii katika C4 mikondo mitatu.
Kila mkondo hautaruhusiwa kuwa na zaidi ya wanafunzi 40. Hii ina maana kuwa shule ya kitaifa haitapokea zaidi ya wanafunzi 400.
Mbunge wa Kitutu Masaba Clive Gisairo, aliyewasilisha hoja hiyo, alisema mpango huo utasaidia kupunguza msongamano katika shule za kitaifa na za mikoa huku ukiongeza idadi ya wanafunzi katika shule za kaunti na za kaunti ndogo.