Ayoub ashiriki mkutano JPC Tanzania, Uganda
DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, ameshiriki Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission – JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda uliofanyika ili kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo jijini Dar es Salaam jana. Katika …
The post Ayoub ashiriki mkutano JPC Tanzania, Uganda first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, ameshiriki Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission – JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda uliofanyika ili kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo jijini Dar es Salaam jana.
Katika mkutano huo wajumbe wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano ya kidiplomasia na kisiasa, masuala ya ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji.
Pia viongozi hao wamejadili maendeleo ya miundombinu ikiwemo sekta za ujenzi, usafirishaji na nishati ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi na kurahisisha biashara kati ya Tanzania na Uganda.
Vilevile, wamejadiliana namna vitambulisho vya uraia vya Tanzania na Uganda vinaweza kutumika kama nyaraka rasmi vya utambulisho wakati wa kusafiri kati ya nchi hizo mbili.
Lengo la hatua hii ni kuhakikisha kwamba vitambulisho vya taifa vinavyotolewa na pande zote mbili vinatambulika pamoja na kuwarahisishia wananchi wa nchi hizo mbili kusafiri kwa urahisi zaidi.
Kikao hicho ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Uganda, pamoja na kuendeleza mahusiano ya kirafiki na kidiplomasia kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.
The post Ayoub ashiriki mkutano JPC Tanzania, Uganda first appeared on HabariLeo.