Amisi ampigia debe Matiang’i, asema kiti cha chini anachoweza kupata ni unaibu wa rais
MBUNGE wa Saboti, Caleb Amisi, amesema kiti cha chini kabisa ambacho kiongozi wa Jubilee, Dkt Fred Matiang'i, anaweza kukubali katika muungano wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027 ni Unaibu Rais, kama si tiketi ya kuwania urais yenyewe.
Amisi alisema hayo alipozuru kaunti ya Kisii mnamo Alhamisi, Septemba 24, kuwa ni kudhalilisha kumzungumzia Matiang'i kwa vyeo vya chini kama Uwaziri, akisema aliyekuwa Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ameshavuka kiwango hicho.
"Mtu kama Fred Matiang'i, kiti cha chini kabisa anachoweza kupewa ni Unaibu wa Rais. Kama si hivyo, basi apewe tiketi ya Urais. Hatuwezi kumzungumzia tena kama mtu wa kupewa Wizara. Amepita hapo," Amisi alisema.
Mbunge huyo alikuwa Kisii kukipigia debe chama chake kipya cha People's Renaissance Movement (PRM) na kujenga uungwaji mkono wa Dkt Matiang'i katika eneo la Gusii.
Kwenye ziara yake, Amisi alikutana na makundi ya vijana na kina mama katika mikutano ya hoteli na ya barabarani maeneo ya Keumbu na Kisii Mjini, ambako alielezea dira ya chama chake na msimamo wake kuhusu mustakabala wa upinzani.
Alisema upinzani unapojipanga kumkabili Rais William Ruto, lazima uonyeshe heshima kwa viongozi wenye uzito wa kitaifa kama Dkt Matiang'i.
"Kuna tabia ndani ya upinzani ya kutaka kumpunguza Matiang'i hadi nafasi ya uwaziri. Hiyo ni dharau kubwa. Mtu aliyesimamia wizara kubwa kama Mambo ya Ndani na Elimu, akaonyesha uwezo wa kipekee, si mtu wa kupewa tena nafasi ya waziri. Ameshavuka hapo," alisema Amisi.
Aliongeza kuwa Matiang'i ndiye kiongozi anayefaa zaidi kuongoza muungano wa upinzani kutokana na uzoefu wake serikalini na mtindo wake wa uongozi unaoaminika.
"Ukizungumzia viongozi ambao wamewahi kuendesha serikali kwa msimamo na nidhamu, Matiang'i yuko juu. Ndiyo maana tunasema kama hatutampatia urais, basi angalau tumpatie unaibu. Chini ya hapo ni kumkosea heshima jamii nzima ya Gusii na Wakenya wanaomuamini," alisisitiza.
Amisi alisema chama chake cha PRM kimejipanga kuzunguka maeneo mbalimbali nchini kuimarisha umoja wa vijana na kina mama ambao ndio wamekuwa wakisahaulika licha ya kuwa na kura nyingi.
Alisema jamii ya Gusii imekuwa na mchango mkubwa katika siasa za taifa lakini imekuwa ikipata nafasi ndogo katika uongozi wa juu, na wakati huu inastahili kupata nafasi kubwa kupitia Matiang'i.
"Gusii imekuwa na kura, imekuwa na viongozi wazuri, lakini haijawahi kupata nafasi ya juu. Wakati huu msikubali makombo. Lazima muwe mezani, na njia ya kuwa mezani ni kumpa Matiang'i tiketi ya juu," alisema.
Kauli ya Amisi inakuja wakati viongozi wa upinzani wakiendelea na mazungumzo ya kuunda umoja mpana wa kumkabili Rais Ruto, huku mgawanyo wa nafasi ukiwa kitovu cha mvutano.