Akili unde kuboresha huduma za kijamii
DAR ES SALAAM: Serikali imesema itaendelea kutumia teknolojia ya Akili Unde (IA) katika kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuongeza ufanisi ndani ya taasisi za umma. Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Mrope, amesema ukuaji wa teknolojia unaendelea kusaidia kutatua changamoto za wananchi, ikiwemo …
The post Akili unde kuboresha huduma za kijamii first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: Serikali imesema itaendelea kutumia teknolojia ya Akili Unde (IA) katika kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuongeza ufanisi ndani ya taasisi za umma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Mrope, amesema ukuaji wa teknolojia unaendelea kusaidia kutatua changamoto za wananchi, ikiwemo kuunganisha mifumo ya Serikali ili iweze kusomana na kurahisisha utoaji wa huduma.
Mrope ameyasema hayo wakati akifungua mdahalo kuhusu matumizi ya Akili Unde katika kuboresha huduma kwa umma.
Amesisitiza kuwa teknolojia imekuwa chachu ya maendeleo kwa kusaidia mifumo mbalimbali, ikiwemo ya ajira, kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Aidha, ameeleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza matumizi sahihi ya teknolojia kama nyenzo muhimu ya kukuza uchumi na kuongeza ushindani wa kimataifa.
Hivyo amezitaka taasisi zenye dhamana ya elimu ya sayansi na teknolojia kusimamia ipasavyo mageuzi hayo ili kuongeza tija.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Ernest Mabonesho, amesema moja ya majukumu ya chuo hicho ni kujadili, kutoa elimu na kubadilishana uzoefu kupitia majukwaa mbalimbali kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi.
Naye, Mkufunzi Jumanne Mtambalike ameshauri sekta zote kuchukua tahadhari na kujiandaa na mabadiliko ya teknolojia, akisema kuwa mageuzi ya kidijitali yataathiri nyanja zote za maisha na kazi.
The post Akili unde kuboresha huduma za kijamii first appeared on HabariLeo.