Ahadi ya Mbadi ya kupunguza ushuru wa PAYE yageuka hewa; haiko kwenye Bajeti 2026

Taifa Leo
Published: May 11, 2026 08:40:54 EAT   |  General

WAZIRI wa Fedha, John Mbadi ameghairia nia kuhusu ahadi ya kupunguza ushuru wa mshahara kwa wafanyakazi walioajiriwa wanaolipwa chini ya Sh50,000.

Kwenye Mswada wa Fedha wa 2026, hakuna ushuru wa mapato ambao utapunguzwa, hili likiwa pigo kwa mamilioni ya waajiriwa ambao wanakumbwa na ugumu wa maisha baada ya mshahara wao kukatwa sana.

Serikali ilikuwa imeahidi kuondoa ushuru kwa Wakenya wanaolipwa mshahara wa hadi Sh30,000 kwa mwezi na kupunguza ushuru kwa mishahara ya chini ya Sh50,000.

Wafanyakazi hao wangepunguziwa kati ya Sh731 na Sh2,127.

Hazina iliachana na Mswada Spesheli wa Marekebisho ya Ushuru 2026 ambao ungesaidia katika utekelezaji wa makato hayo kwa wafanyakazi.

Mswada huo upo bungeni na unatarajiwa kupitishwa kufikia mwisho wa Juni.

“Tumeweka mswada huo kando kwa sababu tuna wiki chache tu kabla ya kuwasilishwa kwa Mswada wa Fedha 2026,” Bw Mbadi aliambia Kamati ya Bajeti bungeni Machi 31.

Badala yake Hazina Kuu imeongeza ushuru wa kodi ya nyumba, simu, pombe, sigara na kamari ili kupata Sh120 bilioni kwenye Mswada wa Fedha wa 2026.

Hii imepanda kutoka Sh30 bilioni ambazo serikali ililenga kwenye Bajeti ya 2025.

Hazina Kuu pia inalenga Sh81 bilioni kutoka kwa watu wasiolipa ushuru. Mamlaka ya KRA inatarajiwa kukusanya Sh2.985 trilioni kanzia Julai.